Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyofanyiwa uchanganuzi wa kisasa. Mabadiliko ya lugha yamechunguzwa katika matawi ya isimu yakiwemo isimu historia na isimujamii. Hata hivyo, tawi la isimu historia halijafanyiwa utafiti wa kuridhisha katika Kiswahili. Makala hii inatoa ithibati ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi katika maneno teule ya Kiswahili. Nadharia ya fonolojia zalishi (FZ) ya Chomsky na Halle (1968) iliteuliwa kuongoza utafiti huu. Mbinu ya uundaji ndani (UN) na mbinu linganishi (ML) zilitumiwa kama malighafi ya kutoa ithibati ya udondoshaji huu. Kwa kutumia mbinu ya uundaji ndani, tofauti za kisinkroniki na ujumbe uliopo kuhusu etimolojia ya neno ulimsaidia mtafiti kuelewa leksika ya sasa. Mbinu linganishi ilitumika kulinganisha maneno ya Kiswahili na mengine ya lugha mnasaba (Ekegusii, Kikuyu, Kiluhya, Kimeru, Kitaita na Kikamba). Mbinu hizi zilijengana na kukamilishana kila moja ikifidia upungufu wa nyingine. Iwapo ushahidi upo kutoka kwa uundaji ndani kama mbinu ya uundaji upya wa leksika, mbinu linganishi ilitumika kuhakikisha usahihi wa ushahidi uliotolewa na mbinu ya uundaji ndani. Isitoshe, pale ambapo mbinu ya uundaji ndani ilikosa kutoa ithibati au kuwa na upungufu, mtafiti alirejelea mbinu linganishi ili kubaini umbo asilia la neno teule la Kiswahili. Data ya maktabani iliwekea msingi upataji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kupitia kwa maswali ya hojaji. Data imechanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo, majedwali na unukuzi wa sheria za kifonolojia. Makala hii ni nafasi bora ya kuchangia katika isimu historia, leksikografia na fonolojia ya Kiswahili.
Mtaala Wa Isimu Pdf Download
2ff7e9595c
Comments